Marekani imeonya kuwa mpango wa Uchina, wa kuanza safari za ndege za raia hadi kisiwa chenye mzozo, katika bahari ya Kusini ya Uchina, unaweza kuzidisha hofu baina ya nchi katika kanda, zinazodai eneo hilo.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani, alieleza kuwa Uchina inafaa kufuata ahadi ilizotowa awali, kuonyesha uvumilivu na iache kupanua visiwa na miamba inayodhibiti.
Nchi kadha za Asia, pamoja na Malaysia, Ufilipino na Vietnam, piya zinadai visiwa hivyo.
Hapo jana shirika la habari la taifa, Xinhua, liliarifu kuwa safari za ndege za kusafirisha raia hadi mji wa Sansha, katika kisiwa cha Woody, zitakuwa zimeshaanza kabla ya mwaka mmoja kumalizika.
Mkutano ulipangwa kufanyika katika jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano.
Mkutano huo ulifutwa pia kutokana na sababu za kiusalama baada ya bwana Trump kukutana na maafisa wanaohusika na masuala ya usalama wa eneo hilo.
Image copyrightReutersImage captionWaandamanaji
Mamia ya watu walikuwa wamekusanyika nje ya chuo ya Illinois saa chache kabla ya bwana Trump kuwasili.
Mapema polisi waliwakamata zaidi ya watu 30 katika mkutano wa Trump katika jimbo la Missouri.
Image copyrightGettyImage captionBaadhi ya waandamanaji walikamatwa
Ndani ya ukumbi wa mkutano huo vita vilizuka kati ya wafuasi wa na waandamanaji ambao walipeperusha bendera na kutoa matamshi.
Taarifa kutoka kampeni ya bwana Trump ilisema kuwa mgombea huo aliamua kufutilia mbali mkutano huo baada ya kukutana na maafisa wa polisi.
Image copyrightReutersImage captionWafuasi wa Trump
Katika mkutano huo kulikuwa na matamshi ya kumsifu bwana Trump kutoka kwa wafuasi wake huku baadhi ya waandamanaji wakitoa matamshi ya kumsifu Bernie Sanders.
Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.
Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.
Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguoza kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji. Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari. Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?” Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini….. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?! Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana. Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: “Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu” “Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto. Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji. “ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka. Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi: “Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.” HEKIMA: 1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE. 2. “TENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILAYA KUJALI HALI ULIYONAYO.
Si rahisi kwa wanamke kukwambia kama anakupenda Bali atakuonyesha ishara kama.....
Nimekuletea ishara chache ambazo waweza kujua kama na wewe unapendwa.
Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupeda kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na haraka kumtolea uvivu huyo mwanamke.* Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke huyo anaupendo na wewe.* Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,Wivu ni ishara kuwa anakupendawewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.Japo wivu ukizidi sana pia inaweza kuleta tatizo.* Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho/uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.* Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa “NJOO NIKO KWAAJILI YAKO.”Hivyo kama ulikuwa unahisi unamhitaji basi ni wakati mwafaka wa kumfuata na kumweleza ukweli na kirahisi nakuhakikishia unabeba mzigo kwani ni mtu tayari aliyekuwa anahisia kali za mahaba juu yako