wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango
kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo
ndani, wakachoma moto baadhi ya magari
yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo
limetokea leo kufuatia mwanamke ambaye
hakufahamika jina lake wakati anakimbia alichotwa
mtama na Polisi na kusababisha mama wa watu
kuanguka na kufariki hapo hapo .
Mama huyo alikuwa anawakimbia polisi waliokuwa
kwenye oparesheni ya kuwakamata watu
wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma
moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda
mikoani na kuyazuia magari kupita, hali
iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa
nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea
kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja
vioo vyake.
![]() |
Basi linalosemekana walikuwepo Askari |
![]() |
Wananchi waliofunga barabara |
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.