Sunday, 13 March 2016

China yaonywa na Marekani kuhusu visiwa


mage caption
Visiwa vinavyopiganiwa na Uchina
Marekani imeonya kuwa mpango wa Uchina, wa kuanza safari za ndege za raia hadi kisiwa chenye mzozo, katika bahari ya Kusini ya Uchina, unaweza kuzidisha hofu baina ya nchi katika kanda, zinazodai eneo hilo.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani, alieleza kuwa Uchina inafaa kufuata ahadi ilizotowa awali, kuonyesha uvumilivu na iache kupanua visiwa na miamba inayodhibiti.
Nchi kadha za Asia, pamoja na Malaysia, Ufilipino na Vietnam, piya zinadai visiwa hivyo.
Hapo jana shirika la habari la taifa, Xinhua, liliarifu kuwa safari za ndege za kusafirisha raia hadi mji wa Sansha, katika kisiwa cha Woody, zitakuwa zimeshaanza kabla ya mwaka mmoja kumalizika.

Mkutano wa Donald Trump wakumbwa na ghasia


Image copyrightAP
Image captionDonald Trump
Mkutano ulipangwa kufanyika katika jimbo la Chicago nchini Marekani wa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump umehairishwa baada ya kutokea maandamano.
Mkutano huo ulifutwa pia kutokana na sababu za kiusalama baada ya bwana Trump kukutana na maafisa wanaohusika na masuala ya usalama wa eneo hilo.
Image copyrightReuters
Image captionWaandamanaji
Mamia ya watu walikuwa wamekusanyika nje ya chuo ya Illinois saa chache kabla ya bwana Trump kuwasili.
Mapema polisi waliwakamata zaidi ya watu 30 katika mkutano wa Trump katika jimbo la Missouri.
Image copyrightGetty
Image captionBaadhi ya waandamanaji walikamatwa
Ndani ya ukumbi wa mkutano huo vita vilizuka kati ya wafuasi wa na waandamanaji ambao walipeperusha bendera na kutoa matamshi.
Taarifa kutoka kampeni ya bwana Trump ilisema kuwa mgombea huo aliamua kufutilia mbali mkutano huo baada ya kukutana na maafisa wa polisi.
Image copyrightReuters
Image captionWafuasi wa Trump
Katika mkutano huo kulikuwa na matamshi ya kumsifu bwana Trump kutoka kwa wafuasi wake huku baadhi ya waandamanaji wakitoa matamshi ya kumsifu Bernie Sanders.