Tuesday, 14 April 2015

Messi na Ronaldo Kucheza Timu Moja



ronaldo messi

Ulimwengu wa soka kwa miaka ya karibuni umetawaliwa na wachezaji wawili toka Fc Barcelona na Real Madrid .
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwa pamoja wamekuwa katika kiwango ambacho kimewafanya waonekane kama watu wanaotoka kwenye sayari nyingine hali ambayo imezua upinzani baina yao ambao kila siku huibuka kwenye mijumuiko ya wapenda soka.
Moja ya hoja ambazo zimekuwa zikiibuka ni nani kati ya wawili hawa ni bora kuliko mwingine , hoja hii imezaa swali linguine miongoni mwa watu ya kwamba ingekuaje kama wachezaji hawa wangekuwa kwenye timu moja .
Ni vigumu kwa hili kutokea kwani kwa sasa wanacheza kwenye timu zenye utamaduni wa upinzani na wanakoelekea ni vigumu kuona wakibadilishana timu siku moja yaani Ronaldo akichezea Barcelona na Messi akichezea Madrid  na hata kwenye timu ya taifa uwezekano huo haupo kwani Messi ni Muargentina na Ronaldo anatoka Ureno .
mundo deportivo
Jarida la Mundo Deportivo limeripoti mpango wa kuandaa mchezo maalum wa wachezaji nyota barani ulaya .

Hata hivyo ndoto ya wawili hawa kuonekana wakichezea timu moja huenda ikawa kweli baada ya jarida moja la Hispania Mundo Deportivo kuripoti mpango wa kuandaa mchezo wa wachezaji nyota toka klabu mbalimbali barani ulaya .
Mpano huu umetokana na wazo kama la mchezo wa wachezaji nyota wa NBA yaani NBA All Star ambapo wachezaji huchaguliwa na kuwakilisha kambi za mashariki na magharibi na kwa ulaya zitachaguliwa timu mbili zikiwakilisha wachezaji oka vilabu vya ulaya kaskazini na kusini.
Wazo hili litahusisha wachezaji watakaochaguliwa na mashabiki kupitia mtandao ambapo kutakuwa na wastani wa wachezaji watatu toka klabu moja na hapa ndio uwezekano wa kuwaona Messi na Ronaldo wakiwakilisha Hispania ambayo iko kwenye eneo la kusini mwa ulaya .
Wachezaji wengine nyota kama Zlatan Ibrahimovic , Gareth Bale , Neymar na Edinason Cavanni pia wanaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha ulaya kusini ambacho kitakuwa na klabu za mataifa ya Ureno , Hispania na Ufaransa .
Wachezaji kama Wayne Rooney , Angel Dim Maria , Sergio Aguerro , Alexis Sanchez na Edin Hazard pamoja na wachezaji nyota wa Bayern Munich watawakilisha kikosi cha klabu za Ulaya kaskazini .
Hata hivyo bado wazo hili halijawa rasmi na haijafahamika kama litafanyiwa kazi kikamilifu na kuweza kutimiza azma ya mashabiki ya kuona mkusanyiko wa wachezaji noyta wakiwa wanacheza kwenye timu moja 

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.