Monday, 6 April 2015

Wamisri wapinga hujuma ya Saudia huko Yemen

Maandamano makubwa yamefanyika nchini Misri kupinga mashambulizi ya anga ya majeshi ya Saudia na nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (PGCC) dhidi ya wananchi wa Yemen.

Waandamanaji mjini Cairo wamekwenda hadi nje ya ubalozi wa Saudia na kulaani mashambulizi hayo huku wakitaka yasitishwe mara moja.

Waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye picha za Mfalme wa Saudi Arabia, Salman bin Abdul Aziz na chini ya picha hizo kuna maandishi yanayosema 'Mamluki wa Marekani'.

Waandamanaji hao aidha wamemtaja balozi wa Saudia nchini Misri kuwa adui wa Wamisri na wamemtaka aondoke katika nchi hiyo mara moja.

Rais wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi, ni miongoni mwa viongozi wa Kiarabu wanaounga mkono mashambulizi ya Saudia dhidi ya watu wa Yemen.

Washauri wa kijeshi na vyombo vya habari vya Misri vimemtahadharisha kiongozi huyo juu ya matokeo mabaya kwa hatua yake ya kuunga mkono hujuma ya Saudia huko Yemen.

Chanzo: kiswahili.irib.ir

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.