Hapa ni Mbezi, Mabasi ya UDA Yalikuja kutoa msaada lakini yamezuiliwa kupakia abiria hivyo milango imefungwa.
=> Mtwara Magari hayakutoka kwenda Dar kwasababu hawajui hatms ya huko Dar ila walikuwa tayari kusafieisha abiria, daladala na magari ya wilayani hakuna.
=> Kuna magari yamezuiwa Chalinze, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele Chalinze wamepigwa mawe.
=> Hapa stendi ya Njombe mabasi hayajaondoka mpaka muda huu.
=> Hapa Mbagala kuna baadhi ya daladala zimeamua kuendelea kuchukua abiria lakini zinavamiwa na madereva wanaoshinikiza mgomo. Wanashusha abiria toka kwenye daladala.
By kivyako:
Niko kituoni hapa mitaa ya Segerea, hakuna gari hata moja abiria tumeduwaa kituoni! Jinsi ya kufika kibaruani haieleweki! Je, huko ulipo hali ikoje?

By Sir Good:
Serikali kupitia Sumatra imekuja na kanuni mpya ya kuwataka madereva kwenda kusoma kila baada ya miaka mitatu, hii inahusu madaraja yote kuanzia A mpaka C. Ada ya kusoma kwenye vyuo vya udereva ni tsh 500,000. Mgomo huo unatokana name kupinga ujinga huo ulioletwa na serikali, hats sisi madereva wa pick up Leo Leo tumegoma! Kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, lengo Leo kisitembee chombo chochote barabarani kuanzia gari, bajaji mpaka bodaboda kwani maumivu ya hiyo sheria yanatugusa wote.

By Pendael24:
Abiria wana pata shida ya ajabu Morogoro, bodaboda ndio zinatoa msaada ila kwa wale wenye uwezo. Wale wenzangu na mie wapo vutuoni hawana lile wala hili, sijui migomo hii ni mpaka lini, Abood Ndio Wakati Wako Wakutoa Msaada Sasa Sio Kwenye Kuzika Tu.

Chanzo: Jamii forum
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.