Sumaye aonya unyanyasaji raia uchaguzi mkuu TZ

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye ameonya kuwa vitendo vya unyanyasaji wa raia yakiwamo mauaji wakati wa Uchaguzi Mkuu, vinaweza kuhatarisha amani na kulifanya taifa kuingia katika machafuko yasiyoweza kuzuiliwa.
Sumaye amesema kwamba, kuna haja kuzidi kuomba amani kwa ajili ya nchi ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani, lakini akaonya kuwa ili kusikilizwa na Mungu, lazima taifa kutubu na kuacha kutenda maovu.
Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kama ninavyomnukuu: "Tusiue watu, tusidhulumu haki za wanyonge, tusitoe wala kupokea rushwa wala kufisadi mali ya umma, tusifanye biashara ya dawa za kulevya na kuharibu watoto wa watu wengine, na maovu mengine mengi katika jamii. Mwisho wa kunukuu.
Kwa mujibu wa Sumaye, mambo ya kuzingatia ili kudumisha amani na utulivu wakati uchaguzi huo wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani ni kuandikisha raia wote wanaostahili kwenye daftari la kudumu la wapiga kura linalopaswa kuwa wazi kwa kila mtu.
Pia amesema wakati wa kampeni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), inapaswa kuhakikisha kuwa haki inatolewa kwa usawa kwa vyama vyote.
Chanzo, kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.