Friday, 20 February 2015

Hutojua thamani yangu mpaka nitoke mikononi mwako.

Wapenzi wasomaji wa blog yetu na simulizi zipatikanazo humu.

Kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu ile simulizi yetu ya "hutoijua thamani yangu mpaka nitoke mikononi mwako "dullah(Abdallah) na hajjat(hajjrah) tutaimalizia leo hapa haitoendelea tena.

Napenda kuwafahamisha wote muliokuwa mnafatilia simulizi hii najua mnataka kujua ni kwanini mwandishi ameamuwa kuandika simulizi hii? 

Jina la mwandishi ni Abdulaziz Ahmad Maalim


Kuna habari zilizonifikia mezani kwangu ambazo hazikunifurahisha na ndo mana nataka nitoe ufafanuzi kuhusu simulizi hii

Kuna baadhi ya wasomaji hawakuielewa simulizi hii inahusu nini na chanzo cha simulizi. 

Kila mtu anamtazamo wake tofauti ambao wengine walijijengea mawazoni mwao.


"Hutojua thamani yangu mpaka nikutoke mikononi mwako"

            Historia kwa ufupi kuhusu simulizi ya "Hutojua thamani yangu mpaka nikutoke mikononi mwako".Hii ni filamu iliyotengenezwa nchini filiphino ambayo nilitumiwa kipande cha video kwa njia ya ujumbe kupitia mtandao wa kijamii  wa whatsapp.Nilipojaribu kuiangalia video hiyo niligundua kitu fulani yaani hisia katika ulimwengu wa mapenzi na kwenye ndoa.

        Nikajaribu kutengeneza fikra furani kichwani kwangu kwa kuongeza vionjo katika video hiyo na kutengeneza simulizi ili ivutie hadhira/wasomaji wa simulizi yangu hii. Hizo ni tekniki (technical) ambazo waandishi wengi hutumia kwa lengo la kuvutia wasomaji katika simulizi zao au vitabu vyao vya hadithi.

         Ila kwangu nilichojaribu kukifanya Mimi ni kutengeneza simulizi hii fupi ambayo itaibua hisia za wapenzi wangu wa simulizi hii.

        Cha kushangaza baadhi ya wasomaji fikira zao zilifika mbali na kuanza kushabihisha simulizi hii na maisha halisi ya mwandishi wa simulizi hii ambayo yaliopita miaka kadhaa huko nyuma na na wengine walifika mbali zaidi kuitafsiri wanavyojua wao.

         Labda nifafanua kwa upande wa wahusika wa simulizi hii ili waweze kupata mwangaza nakuweza kufuta fikra zao juu ya mwandishi.

        Nianze kwa kuwaelezea wahusika wa simulizi hii.

Wahusika:

1.Hajjat.
Ndie mhusika mkuu wasimulizi hii jina lake kamili ni Hajrah bint Abdul-malik.
Alikuwa anamsimulia mwandishi historia ya maisha yake ya ndoa na mitihani iliyomkuta baada ya kumpoteza mume wake Dullah (ambaye ni Abdallah) baada ya kufikwa na mauti kwa kuathirika na msongo wa mawazo kichwani kwake kwa yale aliokuwa akifanyiwa na mkewe (ambaye ni hajjat).


2.Dullah.
Huyu nimuhusika wa pili wa simulizi hii  jina lake kamili ni Abdallah bin Salim.
Ambaye pia ni mhusika mkuu, kiufupi huyu katika simulizi yetu mwishoni alifariki  baada ya kupata maradhi ya moyo na shinikizo la damu kutokana na kunyanyaswa na aliyekuwa mpenzi wake kabla ya kuwa mke wake ambaye ni Bi Hajjat kutoka na mapenzi yao kudorola kwa upande mwengine kiwango cha mapenzi kushuka na kumpelekea Hajjat kutomthamini Dullah mpaka alipopelekwa hospital na mauti yalipomkuta huko huko hospital na ndio sababu ya kupatikana jina la simulizi hii baada ya Dullah kufa na kumuacha Hajjat mpweke huku akitamani Dullah aweze kurudi ulimwenguni ili aishie nae vizuri ila haikusaidia tena maana wahenga wanasema "maji yakisha mwagika hayazoleki" akabaki kuendelea na unyonge wake ambao ulimuathiri mpaka alipokutana na mwandishi  na kumuhadithia historia yake.


3.Abdulaziz.
Huyu nae ni muhusika katika simulizi  pia ni mwandishi wa simulizi hii.
Naanza hapa Abdulaziz alikuwa anatembea pembezoni mwa barabara mitaa ya Buguruni.

Ikumbukwe Mwandishi ametumia jina la Buguruni kwasababu ndipo anapoishi.
Abdulaziz alikua ana simuliwa story na mhusika mkuu ambaye ni Hajjat.




TANBIHI: Vionjo mwandishi alivyoongezea ni kutokana na jamii nyingi kuathiriwa na mapenzi (kupenda).
Kiuhalisia mengi hutokea kweli katika jamii zetu.
        Unapopata fursa ya kuwauliza watu wengi hawakosi kukwambia kama wametendwa na wapenzi wao si mwanaume/si mwanamke na ndio sababu iliyopelekea kuandika simulizi hii.
huo ni ufupisho wa simulizi yetu.


Kuna watu ambao wanashabihisha simulizi hii na maisha ya mwandishi jambo ambalo sio kweli.

       Nimalizie kwa kueka kipande cha video ambayo labda kitaleta maana kwa wale wenye mtazamo tofauti.
Kipande ambacho kinaelezea hali halisi ya simulizi yetu.

Majuto ni mjukuu .

Bonyeza kwenye video



NB:Mwandishi  anapenda kuwafahamisha kwamba katika simulizi hii hajamuhusisha  mtu yeyote bali ni mawazo yake mwenyewe
.
Na mmiliki wa blog hii ni Abdulazizalshirazy peke yake.




By Mwandishi.
Abdulaziz Alshirazy

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.